Wolper Ajivua Kuhusu Miss Tanzania "Sihusiki na Chochote Kuhusiana na Miss Tanzania na Siwezi Kuongelea"

Wolper Ajivua Kuhusu Miss Tanzania "Sihusiki na Chochote Kuhusiana na Miss Tanzania na Siwezi Kuongelea"
Msanii wa filamu nchini na mjasiriamali, Jackline Wolper amedai hausiki na jambo lolote linaloendelea mitandaoni kuhusiana na sakata la zawadi ya Miss Tanzania 2018, kama ilivyoelezwa na muandaji wa mashindano hayo.

Wolper ametoa kauli hiyo leo Septemba 11, 2018 alipokuwa anazungumza na www.eatv.tv baada ya Mratibu wa shindano la hilo na Mkurugenzi wa The Look Company, Bi. Basila Mwanukuzi kunukuliwa katika mahojiano yake aliyoyafaya jana na www.eatv.tv na kudai kuwa, mrembo huyo ndio chanzo wa kueneza chuki pamoja na sifa mbaya juu ya zawadi ya mshindi kutokana na kunyimwa nafasi ya kuwa jaji.

"Sihusiki na chochote kuhusiana na Miss Tanzania na siwezi kuongelea jambo lolote lile ambalo nimetuhumiwa nalo", amesema Wolper.

Mashindano ya kumsaka mlimbwende yalifanyika Septemba 08, 2018 jijini Dar es Salaam ambapo mara baada ya kutangazwa na kujulikana mshindi wa taji la Miss Tanzania 2018 ambaye ni Queen Elizabeth Makune, kulianza kuzagaa picha ya gari mitandaoni ambayo kila mtu alikuwa anaongea lake juu ya hilo huku ikidaiwa kuna baadhi ya watu wachache ndio waliosababisha mambo hayo yote akiwemo Wolper.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad