Wolper Awapa Somo Mastaa

Wolper Awapa Somo Mastaa
STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amebumburua kuwa, huu ni wakati wa mastaa na watu wenye majina makubwa kutupilia mbali maisha feki ambayo wanayaonesha kwenye mitandao ya kijamii.

Katika mazungumzo na Ijumaa Wikienda, Wolper alisema wengi wanajipotosha wenyewe kwa kudanganya maisha waliyonayo, jambo ambalo siyo sawa kwa sababu wanapaswa kubuni vitu vingi vya maendeleo kuliko kujionesha kwenye mitandao kuwa maisha yao ni bomba kumbe hakuna chochote.

“Hakuna kitu ninakichukia kama maisha ya kuigiza kwenye mitandao ya kijamii, ninayachukia kwa sababu ipo siku mtu atakuja kuona maisha yangu halisi ashangae hivyo inapaswa kila mmoja kuishi vile Mungu amempangia na siyo kuigiza, hayo maisha feki tuyatupe kule,” alisema Wolper ambaye pia ni mjasiriamali wa ushonaji nguo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad