Yafahamu Matatizo ya Ngozi yanayotokana na Kunyoa Ndevu na Nywele na Jinsi ya Kujitibu
0
September 20, 2018
Wakati unaponyoa ndevu na nywele, baada ya kunyoa, wakati wa kuota nywele hizo zipo baadhi ya sehemu nywele hushindwa kutoka nje ya ngozi na kuota ndani ya ngozi hali inayopelekea kusababisha uvimbe na vipele.
Zipo aina mbili za mapele yanayotokana na Kunyoa nywele na ndevu.
Magonjwa haya ni kama ifatavyo
1. Acne Keloidalis Nuchae
Acne keloidalis nuchae (AKN) Ni tatizo linalotakana na maambukizi ya bacteria P.Acnes kwenye ngozi baada ya kunyoa,hali inayopeleka vijitundu vya vinyweleo kuziba na kufanya nywele kushindwa kutoka nje ya ngozi na kukulia ndani ya ngozi hivo kusababisha mapele makubwa na makovu. Acne keloidalis nuchae (AKN) mara nyingi hutokea sehemu ya kisogo.
Mbali na kunyoa tatizo hili pia huweza kusababishwa na uvaaji wa kofia.
2.Pseudofolliculitis barbae (PFB)
Tatizo hili huwapata watu wengi, hili hutokea sehemu za kidevu na mashavu. Hii pia husababishwa na kuziba kwa vinyweleo vya ngozi baada ya kunyoa hivo kupelekea ndevu kukulia ndani ya ngozi na kusababisha uvimve kwa juu ya ngozi na baadae makovu meusi.
MATIBABU YA PSEUDOFOLLICULITIS BARBAE (PFB) NA ACNE KELOIDALIS NUCHAE
Kuminya mapele haya kwa maji ya moto kama unakanda ngozi.Hii husaidia ngozi zilizokulia ndani kutoka.
Kutumia dawa.
Dawa kama persol na tretnoin cream zinaweza kutumika,Endapo mapele yamekua makubwa sana basi unaweza tumia hizo dawa na ukaongeza doxycycline ya kumeza.
Pia epuka kuvaa kofia au nguo zinazobana.
Tags