Yanga haipoi, yaichapa African Lyon Kwa Shida


Kikosi cha Yanga kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Bao pekee la Yanga limewekwa kimiani na Yusuph Mhilu mnamo dakika za mwisho za mchezo. 

Yanga wametumia mechi hiyo kama maandalizi ya kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara. 

Katika kipute hicho, Yanga imewakosa nyota wake baadhi akiwemo Kelvin Yondani, Thaban Kamusoko, Juma Mahadhi walio majeruhi na wengine waliokuwa Uganda kwa majukumu ya timu ya taifa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad