Yanga Kufunguka Sakata la Mchezaji Wao Kufungiwa na FIFA

Yanga Kufunguka Sakata la Mchezaji Wao Kufungiwa na FIFA
Uongozi wa klabu ya Yanga leo utaweka hadharani sakata linalomkabili kiungo wao mpya Mohammed Issa Banka, aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar.

Yanga wameamua kuitisha kikao na waandishi wa habari ili kuliweka sawa suala la mchezaji wao ambaye imeripotiwa kuwa amefungikwa kwa miaka miwili na Shirikisho la Soka Africa (CAF) kutokana na matumizi ya sigara bwege 'Bangi'.

Baada ya taarifa hizo kutoka Yanga walikuja na kauli wakieleza kuwa wao hawana mamlaka ya kuliongelea huku wakisema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndiyo lina taarifa zake.

Inawezekana Yanga watakuwa walishakutana na TFF, hivyo tusubirie kikao hicho kitakuwa na yapi ya kuzungumzia kuhusiana na mchezaji huyo ambaye yupo kifungoni mpaka sasa.

Kiungo huyo inaelezwa kwa sasa yupo kwao Zanzibar akijifua mchangani ili kulinda kiwango chake mpaka pale kifungo alichopwa kitakapomalizika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad