Imeripotiwa kuwa klabu ya Yanga imepokea milioni 150 ambazo ni mgao wao wa kwanza wa milioni 600 kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu mkuu wa Yanga, Omary Kaya, amethibitisha kupokea fedha hizo ambazo zinalipwa kwa awamu nne na shirikisho la soka barani Afrika (CAF).
Yanga ilizipata fedha hizo baada ya kufanikisha kuindoa Welayta Ditcha ya Ethiopia katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ushindi huo wa 2-1 dhidi ya Waethiopois umeisaidia Yanga kuvuna milioni hizo za awamu ya kwanza huku zingine zikiwa zinakuja taratibu.
Tayari kikosi hicho hivi sasa kipo jijini Dar es Salaam kikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stad=nd United utakaopigwa Jumapili ya wiki hii.