Imeripotiwa Zaidi ya wananchi 500 wamekwama katika eneo la Bugolora baada ya kukosa usafiri wa kuelekea kisiwa cha Ukara kulikotokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018. Wanachi hao wamekwama kutokana na usafiri kuwa wa shida kwani watu wengi sana wanaelekea eneo hilo wakiwemo viongozi wa Serikali.
Baadhi ya wananchi wamelalamikia Serikali na kuiomba watafute nji mbadala ya kuwasaidia kwenda katika eneo hilo kuiona miili ya ndugu zao. Kwa mujibu wa MCL Digital,mmoja wa wananchi hao amesema huenda asiuone mwili wa kaka yake aliyefariki dunia kutokana na ajali hiyo,hivyo kuchelewa kuto huko kutapelekea asiuone kabisa mwili wa ndugu yake huyo.
” Ninakumbuka ajali ya mwaka 1996 ilipozama meli ya Mv Bukoba baadhi ya watu walishindwa kuitambua miili ya jamaa zao hadi Serikali ikaamua kuwazika kwa pamoja” ameongeza mkazi huyo wa Bugorola :-” Sikutaka hili litokee hivyo tunaiomba Serikali iangalia namna nyingine ya kuitumia Mv Nyehunge ifike hapa maana ipo kule Ukara pamoja na Mv Clarias sasa sijui kwanini haziji huku” Lakini wananchi hao wakilalamika lakini wengine wamesema hivyo vivuko ambavyo viko Ukara inadaiwa havina mafuta.