Zitto Amvaa Majaliwa, ni kuhusu ajali ya MV Nyerere


KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemshukia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kushindwa kuwaadhibu viongozi wote waliohusika na kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere.

Kivuko hicho kilizama Septemba 20 mwaka huu wilayani Ukerewe, Mwanza ambapo mpaka sasa idadi ya watu waliokufa inatajwa kufikia 224 ambapo leo Waziri Mkuu ameongoza mazishi ya kitaifa katika makaburi ya pamoja yaliyopo eneo la Bwisya mkoani humo jirani na ajali ilipotokea.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini aliandika maneno haya, " Kwamba mpaka dakika hii hakuna aliyewasilisha barua ya kujiuzulu, Rais hajawajibisha mtu, badala yake Waziri Mkuu anawapongeza kina Mongella na Kamwele kwa kazi kubwa waliofanya. Kazi ya kuacha KUOKOA na kufanya uopoaji, Waziri Mkuu tunakuheshimu sana lakini kwenye hili si sawa"

" Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista nma Kamwelwe bado mawaziri? Ni masikitiko makubwa kwamba, Serikali ya wanyonge imeokoa mtu mmoja wakati wananchi wenyewe wameweza kuokoa watu 40, hii ni aibu kubwa," Ameandika Zitto



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad