RAPA Mmarekani, 50 Cent, anaendeleza visa vyake dhidi ya wasanii wengine kwa nia ya kuwaumbua kwamba hawana umaarufu au wamefifia kimuziki.
Wiki iliyopita, msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson III, aliibuka na kusema kwamba alikuwa amemfanyia mchezo mbaya mwanamuziki Ashanti ambaye aliuza tiketi 24 tu katika shoo ambayo aliichukua badala ya Teyana Taylor.
Mchezo huo wa kuhujumiana ni kwamba rapa huyo hununua tiketi nyingi za kuingilia kwenye shoo za wanamuziki mahasimu wake na kuziharibu.
Katika kile kinachonekana, rapa huyo ambaye pia ni maarufu kwa jina la Fif, anakifanya katika hujuma hizo ni pale majuzi aliponunua tiketi zipatazo 200 za viti vya mbele katika shoo inayotarajiwa kufanywa na mwanamuziki Ja Rule huko Arlington, Texas, Novemba 9 mwaka huu, ili paonekane kwamba shoo hiyo haikuwa na watu.
Rapa huyo akitoboa njama hizo jana aliposema ametumia Dola 3,000 kuhakikisha kwamba viti vya mbele vya shoo hiyo inayojulikana kama Texas Live, viwe tupu.
Hata hivyo, Ja Rule bado hajajibu hujuma hiyo ya mpinzani wake huyo maarufu na mtunzi wa wimbo wa Get Rich or Die Tryin’ ambayo ameiposti kwenye akaunti yake ya Instagram.
“Nimenunua tiketi 200 za shoo ya Ja,” aliandika katika mtandao huo.
Wawili hao wamekuwa katika bifu la zaidi ya miaka 10 ambapo wamekuwa wakilumbana katika mitandao ya jamii, pamoja na kwamba bado wana mafanikio katika tasnia yao ya muziki.
50 Cent Anaendeleza visa vyake Anunua Tiketi 200 za Shoo ya Rule
0
October 27, 2018
Tags