ACT-Wazalendo Wachukua Maamuzi Magumu ya Kuungana na CHADEMA Kulishambulia Goli

ACT-Wazalendo yaungana na CHADEMA

Chama cha ACT-Wazalendo kimetangaza kutoshiriki kwenye uchaguzi mdogo wa marudio unaoendelea nchini kwa kile walichodai ni matumizi mabaya ya kodi za wapiga kura.

Akizungumza mbele ya wanahabari, Katibu Mkuu wa chama hicho Doroth Semu amesema kuwa kupitia kikao chao cha kamati kuu kilichokaa mwezi Julai, kiliamua kushiriki katika chaguzi za marudio ambapo wameshiriki kwenye chaguzi tatu lakini baada ya kutafakari wakaona wajiondoe.

Semu amesema kuwa wametafakari namna zoezi la uchaguzi mdogo linavyoendeshwa na kuona kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za wapiga kura kwani wanaojiuzulu ndio wanaoshinda chaguzi za marudio.

"Tumeshiriki chaguzi tatu mfululizo, tumekaa tukatafakari na tumeona kuwa kuendelea kushiriki ni kubariki jambo la viongozi kujiuzulu na kurudi tena kwa namna nyingine, hivyo tumejiondoa kwenye uchaguzi mdogo wa Disemba 2, mwaka huu", amesema Semu.

Kujiondoa kwa ACT-Wazalendo katika uchaguzi wa marudio, chama hicho kinaungana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilichotangaza kujiondoa rasmi kushiriki chaguzi ndogo zote zilizotangazwa kufanyika hivi karibuni na chaguzi zozote zitakazofuata zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa madai kwamba tume hiyo inafanya kazi ya Chama Cha Mapinduzi.

Kauli hiyo ilitolewa Septemba 19, na mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe na kuituhumu NEC akidai inafanya kazi ya kuhakikisha chama tawala kinashinda kwa kulazimisha matokeo hivyo hawatashiriki katika chaguzi za marudio kwa kile alichodai kuwa, chama kinapitia maumivu mazingira magumu ya kisiasa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad