Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, kamshina msaidizi wa polisi Sweetbert Njewike, amesema kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili ikiwemo gari dogo mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula iliyokuwa na watu watano pamoja na lori.
Kamanda Njewile amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari ndogo iliyokuwa katika mwendokasi ikijaribu kupishana na lori.
"Gari ndogo mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula ilikuwa ikitokea Dodoma kwenda Shinyanga ikiwa na watumishi wa wizara hiyo, ilikuwa katika mwendokasi na kugongana uso uso na Lori", amesema Kamanda Njewile.
Kamanda amewataja waliofariki kuwa ni wanawake wawili na wanaume watatu na wote wamehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni.