Alichokisema Lulu Baada ya Kuvalishwa Pete ya Uchumba ''Nashukuru kwa Kunichagua''

Alichokisema Lulu Baada ya Kuvalishwa Pete ya Uchumba ''Nashukuru kwa Kunichagua''
Mwanadada Elizabeth Michael  aka Lulu, Jumapili hii ilikuwa siku yake nzuri baada ya kuvalishwa pete mume wake mtarajiwa, Majay.

Hayo amefanyika katika sherehe ya wadogo wa mrembo huyo, ndipo CEO huyo wa EFM, alipoamua kutumia nafasi hiyo kwaajili ya kuvisha pete muigizaji huyo wa filamu ambaye alikuwa kimya toka ahukumiwe miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia Mahakama ya kusabisha kifo cha, muigizaji nguli Steve Charles  Kanumba.

Akiongea muda mchache baada ya kuvalishwa pete, mrembo  huyo alionekana kuwa na furaha iliyopitiliza huku akitoa maneno machache kwa mchumba wake huyo.

“Nashukuru kwa kunichagua, nakupenda, sina mengi ya kuongea zaidi hayo,” alisema Lulu kupitia Cheni TV.

Ndoa ya mrembo huyo inadaiwa itakwenda kufanyika Dubai mwezi November na baada ya hapo watarudi Tanzania kwaajili ya kufanya sherehe ambayo itahudhuriwa na watu wake wa karibu.

Lulu bado anaendelea kutumikia kifungo chache cha nje ambapo kupitia adhabu hiyo anafanya shughuli mbalimbali za kijamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad