Alikiba Afunguka Ukweli "Ni Kweli Wimbo wa Hela ni Wazamani Sio Wimbo Mpya..Nimerekodi 2013"

Alikiba atoa wimbo maalum kwa marehemu
Msanii wa muziki na kipenzi cha wengi kutokea Kariakoo Dar es slaam, Ali Saleh Kiba, ameweka wazi sababu ya kudedicate wimbo wake mpya kwa dancer maarufu ambaye kwa sasa ni marehemu, Emanuel.


Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Alikiba amesema marehemu Ima ndiye mtu ambaye alibuni style za kucheza kwenye wimbo huo na alikuwa akiupenda, na hata alipofariki aliwaahidi wenzake kuwa atauchia wimbo huo kwa heshima yake.

“Nilliifanya nyimbo ya hela zamani sana kama 2013, sasa hivi nataka kuichaia kwa sababu dancer wangu Emmanuel ndiye aliitungia style ya kucheza akawafundisha wenzake wote, bahati mbaya Mungu alimpenda alifariki, na niliwaahidi dancers ambao walikuja kwenye msiba kwamba nitafanya nyimbo kwa sababu Ima alisimamia nyimbo ya hela kwa kiasi kikubwa sana, ahadi yangu nilitaka niitimize kwenye arobaini yake ambayo imepita hivi juzi”, amesema Alikiba.

Hata hivyo Alikiba amesema kwamba kwenye video ya wimbo huo ameweka picha za dancer huyo ambaye kwa sasa ni marehemu, kama kumpa heshima yake.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad