Aliyekuwa Msaidizi wa Mbowe amuunga mkono Rais Magufuli kwa kufanya usafi


ALIYEKUWA Diwani wa Kata ya Mtoni kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Benard Mwakyembe leo ameongoza zoezi la ufanyaji usafi katika kata hiyo huku akisema ni jukumu la kila mwananchi kuunga mkono juhudi za Rais Dk John Magufuli katika kuboresha mazingira yaliyo safi na salama. 

Mwakyembe ambaye pia alikua Makamu Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Dar es Salaam na msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema yeye kama mkazi wa Mtoni na mzalendo wa Tanzania ameamua kuungana na viongozi wengine wa wilaya na kata kuhakikisha wanatengeneza mazingira yaliyo salama lakini pia kuhamasisha mazoezi kwa vijana. 

" Nimeamua kushirikiana na viongozi wenzangu kufanya mazoezi ya pamoja na klabu yetu ya Mtoni Jogging ikiwa ni maadhimisho yake ya miaka sita tangu kuanzishwa kwake, lakini sambamba na hilo tuliendesha kampeni ya kufanya usafi, kupanda miti na kuweka mazingira katika hali ya usalama zaidi, maana magonjwa mengi yanatokana pia na uchafu wa mazingira," amesema Mwakyembe. 

Mwakyembe ambaye alijiuzulu nafasi zake ndani ya Chadema na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM amesema ataendelea kushirikiana na wananchi wenzake katika kuunga mkono juhudi za kimaendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad