Aliyelipua Bomu na Kuua Mamia Ahukumiwa Kifo


Mahakama nchini Somalia imemhukumu kifo mtu mmoja aliyekutwa na hatia ya kutekeleza shambulio la bomu lililoua watu takribani 600 katika jiji la Mogadishu, Oktoba 14 mwaka jana.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa katika siku ambayo Somalia ilikuwa inafanya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kutekelezwa kwa tukio hilo linalotajwa kuwa baya zaidi la kigaidi katika historia ya nchi hiyo.

Katika hukumu yake, Mahakama hiyo imeeleza kuwa kijana huyo aliendesha moja kati ya magari ambayo ambayo yalikuwa yamebeba mabomu yaliyohusika.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na tukio hilo, ingawa wengi wanasadiki kuwa kundi la kigaidi la Al-Shabaab ndilo lililohusika.

Katika hatua nyingine, juzi usiku (Jumamosi) watu 20 waliuawa kwa shambulio la bomu katika mji wa Baidoa ulioko Kusini Magharibi mwa nchi hiyo. Kundi la Al-Shabaab limedai kutekeleza tukio hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad