Amber Lulu Afunguka Mahusiano Yake ya Kimapenzi na Marioo


Msanii wa muziki Bongo, Amber Lulu amefunguka iwapo amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Marioo. 

Wawili hao ambao kwa sasa wanatamba na wimbo wao mpya uitwao Yanamiminika walionekana zaidi pamoja hivi karibuni na kuibua maswali iwapo ni wapenzi. 

"Marioo anaweza kuwa kibenten changu kwani kuna shida gani, sianavutia nini yupo vizuri. Lakini ukiangalia sisi tuna wimbo tayari, so ile ilikuwa tu attention," Amber Lulu ameiambia The Playlist ya Times FM. 

May mwaka huu Amber Lulu alitaja orodha ya wasanii wa Bongo ambao amewahi kutoka nao kimapenzi, wasanii hao ni Barnaba, Aslay, Rammy Galis naYoung Dee.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad