Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemthibitisha Ammy Ninje kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo.
Ninje anachukua nafasi hiyo ambayo ilikuwa ikikaimiwa na Oscar Mirambo ambaye ataendelea na jukumu lake la Afisa Maendeleo wa Soka la Vijana.
Kocha huyo amewahi kuteuliwa kukifundisha kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes).