Polisi watatu akiwamo Mkuu wa Kituo cha Polisi Nguruka-Uvinza, Ramadhan Mdimi wameuawa kwa silaha za jadi ikiwamo mishale pembezoni mwa mpaka wa kijiji cha Mpeta
Askari walifika katika eneo la Ilunde lenye mgogoro wa ardhi kuwaondoa wananchi walioanzisha makazi na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji bila kufuata sheria na taratibu za ardhi tangu mwaka 2004
Wananchi walichukizwa na kitendo cha Polisi kuwapora mazao huku wakichoma moto baadhi ya nyumba wakati wa operesheni ya kuwaondoa katika eneo hilo, iliyofanyika Alhamisi
Mgogoro wa ardhi katika eneo hilo umetokana na kubadilishwa matumizi kutoka ardhi ya kawaida ili iwe ranchi ya uwekezaji hivyo raia wanahisi hawatendewi haki
Aidha, raia wanahoji kwa nini igeuzwe ranchi wakati wanatozwa fedha za michango ya maendeleo ya jamii na wanapiga kura kuwachagua viongozi na kama shida ni mwekezaji, wako tayari walipe gharama ili waachwe waendelee na shughuli zao