Askofu Shoo awajia juu wanaovamia maeneo ya Kanisa

Askofu Shoo awajia juu wanaovamia maeneo ya Kanisa
Mkuu wa Makanisa ya  KKKT Dr.Frederick Shoo  amewashukia baadhi ya watu wanaovamia maeneo ya kanisa na kusababisha uhaba wa maeneo ya kanisa kujenga  huduma za jamii ikiwemo shule na vituo vya afya .

Dk.Shoo ameyasema hayo wakati akizindua ya watoto wenye mtindio wa ubongo iliyojengwa na katika usharika wa Wiri na Karansi .  kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo Compassion na watu wa Ujerumani.

Aidha amesema kumekua na tabia ya baadhi ya watu kutumia nafasi zao vibaya kwa kuvamia maeneo ya kanisa kwa lengo la kujitafutia umaarufu wa kisiasa jambo ambalo  linaathiri maendeleo ya kanisa.

"Tuyaache maeneo ya kanisa tusiyavamie ili tukipata wafadhili tuweze kujenga miradi mbali mbali ambayo itasaidia jamii" Alisema Dk.Shoo

Askofu Dr .Shoo ameitaka jamii kuiheshimu mipata na ardhi ya maeneo yote yanayomilikiwa na kanisa hilo ili kuliwezesha kuendelea kushirikiana na serikali ktk kuwahudumia wananchi ktk sekta mbali mbali zikiwemo za elimu na afya. .

Kiongozi wa Ushirika wa Karansi Mch Joshua Laizer amesema kuwa  darasa hilo limejengwa kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali baada ya kuona watoto wengi wa aina wanakosa elimu na wengine kufungiwa hadi wanapoteza maisha.

Mkurugenzi wa Shirika la Compassion Bi. Agnes Hotay ambalo limeshiriki katika ujenzi wa miradi hiyo ameeleza kuridhishwa kwake ktk utekelezaji wa miradi hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana kutekeleza miradi mingi zaidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad