Baada ya kunusurika kifo Kigwangalla atoa sadaka

Baada ya kunusurika kifo Kigwangalla atoa sadaka
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema ameahidi kuwasomesha wanafunzi watano katika chuo cha Utabibu (Tabora Institute), ikiwa ni kurejesha shukrani kwa Mungu kufuatia kunusurika katika ajali ya gari iliyopelekea kifo cha aliyekuwa mpiga picha wake.

Dkt. Kigwangala ametoa ahadi hiyo akiwa katika moja ya mikutano yake katika jimbo la Nzega Vijijini ambapo amesema amechukua maamuzi hayo ikiwa ni kutoa sadaka kwa tukio lililomtokea.

Matokeo ya ajali ile ingeweza kuwa mbaya zaidi kuliko haya niliyoyapata, sina la ziada bali ni kumshukuru mungu kwa kutoa sadaka ya kuwasomesha watoto 5 zaidi pale Nzega mjini pamoja na kusomesha watoto wasiojiweza katika jimbo la Nzega Vijijini''. Amesema Kigwangalla

Aidha Kigwangalla amesema “nitawakatia bima ya afya wakina mama na wazee ili wawe na uhakika wakupata huduma ya afya, nimeshaanza mchakato wa kuwatambua watu wenye uhitaji na hivi karibuni nitatoa msaada wangu.”

Agosti 4 mwaka huu  Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla alipata ajali mbaya ya barabarani katika kijiji cha Magugu Mkoani Manyara baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka na kupelekea kifo cha aliyekuwa Afisa Habari wake Hamza Temba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad