Mdimu alisomewa mashtaka mawili ya kumpa ujauzito na kufanya mapenzi na mwanawe wa kumzaa ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza (jina la shule linahifadhiwa) na mwendesha mashtaka wa polisi, Harrison Chalamila, mbele ya Hakimu Mkazi LilianLutehangwa.
Chalamila alidai juzi kuwa mshtakiwa alianza kufanya mapenzi wa mtoto wake huyo Septemba, mwaka jana, wakiwa wanaishi shambani katika kijiji cha Kitivo wilayani Lushoto.
Alidai kuwa mshtakiwa alipomaliza shughuli za kilimo, alirudi nyumbani kwake katika kijiji cha Masuguru wilayani Muheza anakoishi akiwa na mwanawe huyo na kuendelea na tabia hiyo.
Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa kutokana na kitendo hicho, Aprili, mwaka huu, familia ya jirani na Mdimu ilishtukia kitendo hicho na kuamua kumpeleka katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza kwenda kumpima na ndipo ilipobainika kuwa ana ujauzito.
Baada ya hapo, Chalamila alidai kuwa familia hiyo ilimbana binti huyo amtaje mhusika na ndipo alipomtaja baba yake mzazi.
Alidai kuwa baada ya binti huyo kueleza hivyo, familia hiyo ilikwenda katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Muheza na kutoa taarifa ndipo mtuhumiwa alianza kusakwa lakini alitorokea kusikojulikana.
Hata hivyo, mwenesha mashtaka alidai kuwa jitihada za polisi zilifanikisha kumkamata na hatimaye kumfikishamahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
Katika kesi hiyo, mtoto huyo alitoa ushahidi mahakamani hapo akiwa na ujauzito wa miezi saba, huku akidai kuwa aliyehusika na kitendo hicho kilichosababisha kukatisha masomo ni baba yake mzazi.
Hakimu aliamuru mtuhumiwa kupelekwa mahabusu katika Gereza la Maweni jijini Tanga hadi Oktoba 18, mwaka huu kesi itakapotajwa.