
yeye mwenyewe hakusoma hata darasa moja.
Akizungumza na www.eatv.tv Mzee Rutakwa Lubonankede amesema alishindwa kusoma kutokana na hali ya nyumbani kwao ambapo baba yake alimlazimisha kuacha shule ili kusaidia kazi za nyumbani.
“Kiukweli mimi sikusoma hata darasa moja kwa hiyo sababu kubwa ilikua baba yangu alikuwa mzee sana, nilipopata mtoto nilitamani awe msomi kama wasomi wengine, ndio nikaamua kupeleka wanafunzi watatu pale”, amesema Rutakwa Rubonankede.
Aidha mzee Rutakwa Rubonankede amesema juhudi za mtoto wake aliziona tangu alivyokuwa mdogo kutokana na namna anavyopangilia ratiba pamoja na kujituma kwenye masuala ya masomo.
“Kilichomuwezesha ni kujituma na kila kazi alikuwa anaipenda na mimi nilikuwa nampongeza sana, ndio maana imemuwezesha kufanya vizuri kwenye masomo yake", ameongeza.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Charles Msonde alitangaza matokeo ya darasa la saba jana Jumanne, ambapo katika orodha ya wanafunzi ya waliofanya vizuri Ndemezo Rutakwa kutoka shule ya msingi Kadama mkoani Geita alitangazwa kuwa wakwanza kitaifa.