Baraza la Wazee Chadema Lasema Wanaohama Upinzani Wanashinikizwa

Baraza la Wazee Chadema Lasema Wanaohama Upinzani Wanashinikizwa
BARAZA la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limesema hatua ya baadhi ya viongozi na wanachama wa vyama vya siasa kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kunatokana na shinikizo kutoka katika chama hicho tawala.



Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Kimataifa, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema, Hashim Juma Issa,  amesema baadhi ya viongozi huzushiwa kesi kwa lengo la kuwatishia ili wahamie chama tawala.



Katika hatua nyingine baraza hilo limelalamikia ukosefu wa huduma bora za afya kwa wazee na wastaafu hapa nchini kama, kauli iliytolewa na katibu wa baraza hilo,  Rodrick Lutembeka.



Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee iliyotengwa na Umoja wa Mataifa huadhimishwa kila Oktoba Mosi duniani kote ambapo wazee huitumia siku hiyo kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu wazee.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad