Basi la New Force Lapata Ajali Likiwa Mlima Kitonga


Lilikuwa linaelekea mkoani Dar es Salaam likitokea mkoani Mbeya lilipopata ajali katika mlima huo mkoani Iringa

Kaimu Kamanda Polisi wa mkoa, Deusdedit Kashindo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema watu 10 wamejeruhiwa

Wanne kati ya majeruhi ni Wanaume, watano ni Wanawake na mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na mwaka mmoja na nusu hadi miwili

Majeruhi wawili ambao hali zao si nzuri wamepelekwa Hospitali ya Rufaa Iringa na wengine wanatibiwa katika hospitali ya Wilaya Ilula

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad