Bavicha si Wapinzani Wetu - UVCCM


Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM Taifa, Raymond Mwangwala amesema umoja huo unatarajia kuwa wakala wa kutafuta ajira kwa vijana ili kukabiliana na malalamiko ya ajira hasa kwa vijana nchini.

 Akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast kinachoruka East Africa Radio kuanzia saa 11 Alfajiri, Katibu Mkuu huyo amesema programu hiyo itahusisha vijana zaidi ya mia tatu nchi nzima ambao watapatiwa mafunzo maalum na  ujuzi mbalimbali ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kutumia sekta mbalimbali za kiuchumi.

"Tuna malengo mengi tunayotaka tuyafanye ikiwemo kuangalia ajira kwa vijana, program ya vijana 300, nikuangalia wana ajirika kwa namna gani, kuna makampuni tumeongea nayo na wako tayari tusambaze ajira zao, kwa hiyo lazima uwe na vijana ambao unajua wana sifa gani." Amesema Katibu Mkuu UVCCM Raymond Mwangwala".

Aidha Katibu Mkuu huyo amezungumzia matumizi ya neno UVCCM mpya, Kisarawe mpya, na CCM mpya kuwa hailengi kuonesha viongozi waliopita hawakufanya chochote bali ni kuleta morali kwa wanachama wao.

"Kauli mbiu ilianzia kipindi hichi cha mabadiliko, ni lazima tuje na vitu vipya, ndio maana tumekuja na kauli mbiu na CCM mpya, lengo lake ni kujenga ari mpya kwa wanachama, ndio maana tumekuwa CCM inayotekeleza, sio ya propaganda na slogani huwa zinabadilika kulingana na wakati." amesema Raymond.

Pia kuhusiana na wapinzani wao Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA), Katibu Mkuu huyo amedai kuwa " baraza hilo limekuwa halijihusishi na masuala ya kiuchumi, bali wamejikita zaidi kwenye masuala ya matukio yanayotokea."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad