Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) amesema hawawezi kushindana na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM kwa kile alichokidai umoja huo ni kushindwa kukemea baadhi ya mambo ambayo wao wanaamini hayaendi sawa.
Patrick Ole Sosopi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv iliyotaka kujua kauli yake baada ya Katibu Mkuu wa UVCCM taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala kudai baraza hilo si washindani wao na wanafanya kazi kwa matamko.
Sosopi amesema "Sisi ni baraza kivuli la vijana, ni kweli hatuwezi kushindana na UVCCM kwa sababu ni taasisi ya watoto wa viongozi, ni jambo lipi umesikia wamelikemea ambalo lipo kinyume na haki za kibinadamu wao wakati wote wamekuwa wakiunga juhudi",
Mwenyekiti huyo wa BAVICHA ameendelea kusema "UVCCM wenyewe wako ndani ya chama hicho lakini kila siku wanaunga juhudi wanatofauti gani na wabunge wanao nunuliwa lakini si kusema kuna jambo wamelisema kwa manufaa ya taifa, ni jambo gani walishawahi kusema wako kinyume na viongozi wao".
Jana, 25 Oktoba, Katibu Mkuu wa UVCCM taifa Raymond Mwangwala alidai kuwa "baraza hilo limekuwa halijihusishi na masuala ya kiuchumi, bali wamejikita zaidi kwenye kufuata mkumbo kutokana na matukio yanayotokea".
BAVICHA yaijibu UVCCM, "Hatuwezi Kushindana ni Taasisi ya Watoto wa Viongozi ni jambo lipi wamelikemea"
0
October 26, 2018
Tags