Bilionea mmiliki wa klabu ya Leicester City FC amethibitishwa kuwa miongoni mwa watu waliofariki katika ajali ya helikopta karibu na uwanja wa klabu hiyo Jumamosi.
Klabu hiyo imethibitisha kuwa Vichai Srivaddhanaprabha, 61, kutoka Thailand, wafanyakazi wawili wake, rubani na abiria mmoja walifariki baada ya ndege hiyo kuanguka mwendo wa saa mbili unusu usiku.
Walioshuhudia wanasema ndege hiyo ilikuwa tu imemaliza kuondoka uwanjani pale ilipoanza kuyumba na kuanguka na kuwaka moto.
Maelfu ya watu wameweka maua na skafu za ukumbusho nje ya uwanja wa King Power, na pia ujumbe wa kuwafariji waliofiwa.
Polisi wa Leicestershire wamesema waliofariki duniani wanaaminika kuwa:
Katika taaluma yake, alikuwa ameendesha helikopta zinazotumiwa na vyombo vya habari kufanya matangazo ya moja kwa moja.
Miongoni mwa mashirika aliyoyafanyia kazi ni Channel 4 katika kipindi chao cha The Big Breakfast na pia amewafi kufanyia kazi kipindi cha Virgin Radio.
Lucie Morris-Marr, rafiki yake Swafer, amesema alikuwa rubani mzoefu sana na bila shaka angefanya kila aliwezalo kuzuia ajali hiyo.
Ameongeza kwamba alikuwa mtu mcheshi ambaye alikuwa kwenye mapenzi na Bi Lechowicz ambaye walikuwa wanafanya kazi naye.
"Sio watu wengi huamka na kusafiri na wapenzi wao, wakisafiri maeneo mbalimbali duniani na baadhi ya kifahari," alisema.
Wawili hao wapenzi walikuwa marubani na walikuwa wakiishi pamoja Camberley, Surrey.
Bilionea Mmiliki wa Leicester City Athibitishwa Kufariki Katika Ajali ya Helikopta
0
October 29, 2018
Tags