Bilionea wa Facebook Atumia Kwaajili ya Kujilinda Asiuawe

Bilionea wa Facebook Atumia Kwaajili ya Kujilinda Asiuawe
MWAKA 2017, kampuni ya mtandao wa Facebook ilitumia Dola 7.3 (Sh. bil. 16.7) kwa ajili ya usalama wa Mtendaji Mkuu wake (CEO), Mark Zuckerberg, kiwango ambacho kiliongezeka kwa karibu asilimia 50 kikilinganishwa na mwaka wa nyuma yake.

Hili lilitokana na ziara ya Zuckerberg ya kuzuru kila jimbo nchini Marekani.  Dola 7,326,640 zilizotumiwa na Facebook kuhusu usalama wa bosi wake katika mwaka huo zilikuwa zimeongezeka kutoka Dola 4,891,441 mwaka 2016 na Dola 4,256,004 za mwaka 2015.

Vilevile, gharama za usafiri wake ziliongezeka kwa kiasi kikubwa.  Mnamo 2017, Facebook ilitumia zaidi ya Dola mil. 1.5 kwa gharama za usafiri wa ndege ndege kwa bosi wake huyo kijana mwenye umri wa miaka 33, ambapo ziliongezeka kwa asilimia 75 ikilinganishwa na mwaka 2016 zilipokuwa Dola  mil. 870,000.

Pamoja na takwimu hizi za matumizi makubwa,  Zuckerberg alilipwa mshahara wa dola moja tu mwaka 2017, ikilinganishwa na  Dola 805,000 zilizolipwa kwa Sheryl Sandberg au Dola 720,000 alizolipwa ofisa uzalishaji, Chris Cox.

Hata hivyo, si kwamba Zuckerberg hana fedha kwani jarida la Forbes limeukadiria utajiri wake kuwa chini  kidogo ya Dola bil. 66 ambazo ni sawa na Sh.tril. 151.

Image result for Zuckerberg's security AND BODYGUARDS
“Tunahitaji hatua hizi za usalama kwa faida ya kampuni kutokana na umuhimu wa Zuckerberg kwenye Facebook, na tunaamini kwamba mpango huu wa usalama ni wa lazima.  Tulilipia gharama zote zinazohusiana na usalama wa makazi binafsi ya  Zuckerberg ikiwa ni pamoja na za walinzi,” inasema taarifa kutoka kampuni hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad