Bobi Wine Anena Mazito Kuhusu Museveni

Bobi Wine Anena Mazito Kuhusu Museveni
“Hapana jambo lolote binafsi kati yangu na Museveni,” amesema mwanamuziki wa Uganda aliyejikita katika siasa, Robert Kyagulanyi, na kuongeza “… hizi ndizo hisia ninazokuwa nazo tunapokutana.  Kwa kweli, huwa naushika mkono wake kwa heshima kama Rais wa Uganda.”



Mwanamuziki huyo aliyasema hayo jana katika kipindi cha Side Bar kinachorushwa na kituo cha televisheni cha NTV nchini Uganda.

“Sipendi mapambano haya yakawa kati yangu na Rais Yoweri Museveni tu.  Suala hili ni zaidi yetu wawili na majadiliano lazima yajumuishe Waganda wote,” alisema na kuongeza kwamba iwapo demokrasia inayosemwa nchini ni kupigwa wakati unaendesha kampeni, basi hiyo ni ‘democrazy’, yaani demokrasia ya wazimu.



“Nilikuwa nafurahia maisha ya muziki na kutengeneza fedha nyingi.  Siku moja nilishambuliwa kikatili kwa kuendesha gari la bei kubwa.  Hili ndilo lilinifungua macho na kuuona udhalimu,” alisema na kuongeza kwamba baadaye aliamua kwenda mbele zaidi ya kuimba tu na kuchukua hatua dhidi ya hali hiyo.

Bobi amesema uhuru huja kwa wale wanaoupigania si kwa wale wanaolia, na akaongeza kwamba Uganda imekuwa nchi ya kijeshi.

“Unavyozidi kulia, ndivyo watu wako wanavyozidi kufa, hivyo amkeni mpiganie haki zenu,” alisema.

Akisisitiza kwamba aliahidi kutokuwa mtumwa katika nchi yake, Bobi alisema Waganda lazima wapambane dhidi ya udhalimu katika kila hali.

“Simameni na mseme, hili ni suala la kikatiba.  Lazima tuthaminiwe na kuheshimiwa.  Mustakabali wetu lazima uwe wa uhakika,” alisema.

“Sipendi tukafika hapa, lakini niliahidi kamwe sitakuwa mtumwa… Nikihisi kutotendewa haki, nitapigana kwa muda wote nikiwa hai,” alisema na kuongeza kwamba sasa familia yake inaishi kwa woga kila siku.

“Ni jambo gumu lakini wanafahamu ninachofanya ni cha haki.  Kila siku Mungu ananibariki kwa kuniongezea siku moja zaidi.  Kila siku ninaishi kama vile ndiyo siku yangu ya mwisho.”

Related image


Vilevile, Bobi aliwasifia wananchi wa Kenya ambapo Agosti 23 mwaka huu waliandamana jijini Nairobi wakiwa wamevaa T-shirt na blauzi nyekundu huku wakipiga makelele kumtaka Museveni amwachie Bobi bila masharti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad