Bobi Wine Awabipu Polisi Uganda Aandaa Tamasha Kubwa la Kihistoria

Bobi Wine Awabipu Polisi Uganda Aandaa Tamasha Kubwa la Kihistoria
Msanii wa muziki nchini Uganda ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kyadondo, Bobi Wine amekuja na tamasha lake ambalo litakuwa ni la kihistoria.



Tamasha hilo la kila mwaka linalojulikana kwa jina la Kyalenga, kwa mara ya kwanza litafanyika katika Uwanja wa Taifa wa mpira wa miguu nchini humo wa Namboole.

Akielezea kwa ufupi kuhusu tamasha hilo, Mke wa Bobi Wine, Barbie Kyagulanyi ambaye ndiye meneja wa tamasha hilo, amesema kuwa atasindikizwa na wasanii wenzake kama Eddy Kenzo na wengineo.

Kuhusu sababu ya kuhamisha tamasha hilo ambalo miaka yote hufanyika katika viwanja vya Busaabale, Bi. Barbie amesema kuwa amefanya hivyo baada ya kupata maombi mengi kutoka kwa wadau wa muziki nchini humo.

Bi. Berbie amesema mume wake kwa sasa ni mzima na mwenye afya na ameahidi kujaza uwanja huo unaotosha mashabiki 45,000 .

Katika historia ya muziki nchini Uganda haijawahi kutokea msanii wa nchi hiyo hata mmoja kutumbuiza kwenye uwanja huo. Msanii wa mwisho kutumbuiza kwenye uwanja huo alikuwa ni Lucky Dube.

Kuhusu show hiyo kiujumla, Mke wa Bobi Wine amesema mumewe atatumia dakika 10 kuzungumza na mashabiki wake yote yaliyomtokea mwezi mmoja uliopita, baada ya kukamatwa na kuteswa na jeshi la nchi hiyo kabla ya kuanza kutumbuiza.

Tamasha hilo litafanyika Oktoba 20, 2018 na viingilio ni kuanzia shilingi 10,000/= na VIP tiketi zitauzwa kwa 30,000/= kwa shilingi ya Uganda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad