Bodaboda Wanaoingia Mjini Kukiona

Bodaboda wanaoingia mjini kukiona
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema jeshi hilo linaendesha msako maalum wa kuwakamata madereva bodaboda ambao watakuwa wakifika mjini ikiwa ni kinyume na taratibu za sheria za jiji.


Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa madereva wa bodaboda wamekuwa wakisababisha kutokuwepo kwa hali ya utulivu katikati ya jiji na wakiendelea kuvunja sheria za usalama barabarani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda Mambosasa amesema kwa kipindi cha Masaa 24 wamekamata bodaboda 104 kwa kosa la kuingia kati kati ya Jiji na kubainisha wengine wakizoea adhabu ya faini badala yake watawafikishwa mahakamani.

“Tumeandaa oparesheni kali ya madereva wanaokaidi amri ya kuingia mjini, na mpaka sasa tumeshakamata pikipiki 104 kwa mikoa Kinondoni,Temeke, na Ilala, jeshi la polisi tunapiga marufuku kupita njia ambazo haziruhusiwi kupita, pikipiki hazitakiwi kuingia katikati ya mji ili kulinda hali ya usalama kati kati ya mji.” amemema Mambosasa.

Aidha Kamanda Mambosasa amesema Jeshi hilo kwa kushirikiana Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawashikiria wahalifu 60 kwa kosa kujiunganishia kwa umeme bila kufuata taratibu za shirika hilo hivyo kuhesabiwa kama wahujumu uchumi.

“Wote wanaojihusha na uharibifu wa miundombinu ya Tanesco watafikishwa mahakamani, na sasa tumewakamata waharifu wapatao 60 waliokuwa wakifanya wizi wa mita, kwa nia ya kukwepa gharama za umeme na nawaambia tutawafikia wengine kwa jinsi tunavyokwenda.” amesema Kamanda Mambosasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad