Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa ambaye alijiweka kando kutokana na sababu za kiafya huku nafasi yake amekaimu Omary Kaya amesema kuwa ataweza kurejea Yanga baada ya muda aliojiwekea kupita.
Mkwasa ambaye alifanyiwa upasuaji wa moyo mwanzoni mwa Agosti,mwaka huu anatarajiwa kurejea tena nchini India Novemba 6 mwaka huu kwa ajili ya kufanyiwa vipimo huku akisema kuwa anaendelea vizuri.
"Hali yangu imezidi kuimarika kwani nazingatia masharti yote niliyopewa na dokta, pia nahudhuria kliniki kwa dokta Lwakatare, natarajia kwenda India tena kufanyiwa chek up katika hospitali ile ya mwanzo.
"Kuhusu kurejea Yanga nitaangalia baada ya miezi sita kupita ndipo nitaamua, kwa sasa nimewekeza nguvu yangu kwenye afya, " alisema.