BREAKING NEWS: Mahakama yatupilia Mbali Rufani ya Viongozi tisa wa Chadema

Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5.2018 imetupilia mbali Rufaa iliyofunguliwa na viongozi tisa wa Chadema akiwamo mwenyekiti wake Freeman Mbowe kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu dhidi ya mwenendo wa kesi ya uchochezi unayowakabili katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu sababu taarifa ya kusudio Ia kukata rufaa hiyo inamapungufu kisheria. Mapema mwaka huu, Mahakama kuu ilitupilia mbali maombi ya viongozi hao ya kutaka kufanya marejeo mwenendo wa kesi hiyo kwa sababu ya kuwepo mapungufu kisheria.

Rufaa hiyo ni mwendelezo kutokana na kesi ya msingi ya jinai inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo wanapinga uamuzi na amri mbalimbali ambazo mahakama hiyo imekuwa ikizitoa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad