Leo Oktoba 31 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT -Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi wa Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam muda huu.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Mawasilano ya Umma ya Chama hicho imeeleza kuwa Zitto Kabwe amekamatwa na polisi ili kwenda kuhojiwa Juu ya mauaji ya Polisi na Raia yaliyotokea kwenye Kijiji cha Mpeta, Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, mauaji ambayo alitaka Jeshi la Polisi liyatolee maelezo katika mkutano wake na Wanahabari juzi Jumapili, Oktoba 29, 2018.
Tutawajuza Kila kinachoendelea Wakati huu ambapo Mawakili wa Chama wakishughulikia suala lake aliongeza Ado Shaibu