Breaking:Rais Magufuli aagiza kusimamishwa kazi makamanda wa Polisi
3
October 09, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Kamanda wa Polisi wanne kufuatia tuhuma za kuhusika katika magendo ya zao la kahawa katika Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera pamoja na tuhuma nyingine.
Viongozi hao wa Polisi wanaosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kyerwa, Justine Joseph, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kyerwa, Everist Kivuyo na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kyerwa, Robert Marwa.
Aidha, Rais Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mej. Jen Jacob Kingu na Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika na hatua stahiki zinachukuliwa endapo watabainika kuhusika katika magendo ya kahawa na makosa mengine kwa mujibu wa sheria.
Tuhuma dhidi ya viongozi wa polisi katika Wilaya ya Kyerwa zimebainika jana wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa.
Tags
Kwa nini usimfukuze kazi Makonda, hao wengine unawaonea tu, tungekuchagua, kwa haya unayofanya, tusingekuchagua tena, lakini hujali, kwani umewekwa na uongozi unakushinda. Watu wanapotea upo kimya, Makonda kawa mungu mtu, unacheka tu,,moto wako, power is power..Dar umekuwa mji hataji, mkuu wa mkoa yupo tu. Historia itawakumbuka.!
ReplyDeleteWananuka damu za watu hawa watu..
ReplyDeleteWabaya wetu ni CCM, tuamke tuwatoe hawa wrzi!
ReplyDelete