CCM kususiwa Zanzibar

CCM kususiwa Zanzibar

Chama Cha Wananchi  (CUF) upande Zanzibar kimesema kitaendelea na msimamo wa kutoshiriki Chaguzi mbalimbali zitakazofanyika kwenye visiwa hivyo vya Zanzibar mpaka itakapofika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

 Cuf imesema haitashiriki Uchaguzi wowote hasa upande wa wawakilishi wa majimbo ya Zanzibar kwa kile walichokidai kushiriki chaguzi hizo ni kuhalalisha matokeo ya Uchaguzi wa marudio ya Urais ya uliofanyika machi 20 mwaka 2016 ambapo chama hicho kupitia mgombea wake  Maalim Seif Sharif Hamadi kilisusia.

Akizungumza Naibu Mkurugenzi wa Habari CUF Mbarara Maharagande amesema chama hicho hakija msimamisha mgombea yeyote kwenye marudio ya Uchaguzi wa kupata mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe licha ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza kumsimamisha.

“Kama chama msimamo wetu ni kwamba hatutashiriki uchaguzi wa Jang’ombe, sababu uchaguzi huo umetokana na uchaguzi haramu wa machi 20 2016, kwa hiyo hatutashiriki uchaguzi wowote, utakaoitishwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) isipokuwa Uchaguzi wa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ulitokana na matokeo halali ya kura.”amesema Maharagande.

Katika Uchaguzi wa Jang’ombe Chama cha Mapinduzi kinatarajiwa kupata ushindi mkubwa kufuatia Chama hicho  kumsimamisha Ramadhani Hamza Chande kuwa mgombea kufuatia aliyekuwa mbunge wa Chama hicho kuvuliwa uanachama kwa makosa ya nidhamu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad