CHADEMA Yadhibitisha Kujiuzulu Kwa Mwenyekiti wake


Baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini kujiuzulu jana na kujivua nyadhifa zote ndani ya chama na kutangaza kuwa atajiunga na CCM, CHADEMA imesema kuwa imesikia taarifa hizo kupitia

Akizungumza na www.eatv.tv Katibu wa BAVICHA mkoa wa Mara Yohana Kaunya, amesema kuwa taarifa hizo ni za kweli lakini hajapata barua rasmi kutoka kwa Porini lakini aliona kupitia vyombo vya habari kuwa ametangaza kujiuzulu.

"Nimeona kupitia vyombo vya habari na sijaona barua yoyote ofisini kwangu, nategemea ataleta barua", amesema Kaunya.

Porini ambaye alikuwa diwani wa kata ya Natta na Mwenyekiti wa kijiji cha Makundusi anakuwa diwani wa nne toka aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Marwa Ryoba kujivua nafasi hiyo na kuhamia Chama hicho Septemba 27 mwaka huu.

Kujivua kwake kunaifanya halmashauri hiyo kukosa Mbunge, Mwenyekiti na Makamu wake ambao wote wamehamia CCM wakidai kuunga mkono jitihada za Serikali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad