CHADEMA Yaendeleza Mgomo

CHADEMA yaendeleza mgomo
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kinaendelea na msimamo wake wa kutoshiriki chaguzi ndogo za marudio mpaka pale tume ya taifa ya uchaguzi itakapobadili mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi.


Akizungumza na www.eatv.tv, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na mambo ya Nje, John Mrema amesema kuwa chama hicho kipo kwenye maandalizi ya uchaguzi wa ndani ya chama, na kusisitiza kuwa hawatoshiriki kwenye uchaguzi mdogo katika majimbo ya Serengeti, Ukerewe, Simanjiro na Babati.

Mrema amesema kuwa, "Msimamo wetu haujabadilika hatutashiriki kwenye uchaguzi kwakuwa tumeshuhudia bado uvunjwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi katika chaguzi zilizopita".

CHADEMA kilitangaza kujiondoa rasmi kushiriki chaguzi ndogo zote zilizotangazwa kufanyika hivi karibuni na chaguzi zozote zitakazofuata zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa madai kwamba tume hiyo inafanya kazi kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi.

Kauli hiyo ilitolewa Septemba 19, na mwenyekiti wa CHADEMA  taifa, Freeman Mbowe ambapo aliituhumu NEC akidai inafanya kazi ya kuhakikisha chama tawala nchini ya kinashinda kwa kulazimisha matokeo hivyo hawatashiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Liwale na kata 37 kwa kile alichodai kuwa, chama kinapitia maumivu mazingira magumu ya kisiasa.

Oktoba 18, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salum Mbarouk ametangaza uchaguzi mdogo kwenye majimbo mawili na kata 26 za Tanzania Bara ambapo utafanyika Disemba 2, 2018 katika majimbo ya Babati Mkoani Manyara na Ukerewe jijini Mwanza, ambapo uchaguzi huo utafanyika sambamba na uchaguzi wa jimbo la Simanjiro na Serengeti pamoja na kata 21 za Tanzania Bara uliotangazwa awali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad