Baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kuwahoji wabunge wake wa Moshi Vijijini Antony Komu na Saed Kubenea wa Ubungo kuhusu kuvuja kwa sauti wakipanga njama za kumuondoa Meya wa Ubungo Jacob Boniphace,
CHADEMA wameazimia kuwavua nyadhifa zote za uongozi ndani ya chama
Akizungumza na wanahabari, Naibu Katibu Mkuu Bara John Mnyika amesema kuwa, Kamati Kuu ya chama iliwaita wabunge hawa kuja kujieleza juu ya tuhuma ya utovu huo wa nidhamu, na walifika kujieleza, na walikiri kwamba ni sauti zao.
Mnyika amesema Kamati kuu imewakuta na hatia, imefanya maamuzi ya adhabu juu yao, "mosi imefikia uamuzi wa kuwapa onyo, pili imewataka waandike barua ya kuomba radhi kwa chama., tatu Kamati kuu ikafikia uamuzi wa kuwaweka kwenye uangalizi kwa miezi 12, na nne ikafikia uamuzi wa kuwavua nafasi zao zote za uongozi ndani ya chama na kubaki na ubunge"
Pia wabunge hao Antony Komu na Saed Kubenea ambao pia wamehudhuia mkutano huo, wametakiwa kujitokeza mbele ya umma na kuomba radhi.