Chanzo cha Ajali ya Basi la TASHRIFF Pasua Kichwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema jeshi hilo bado linaendelea kuchunguza chanzo cha ajali ya moto iliyolihusisha gari la kampuni ya TASHRIF mkoani Tanga ambalo halikuleta madhara yeyote.

Mapema leo asubuhi kupitia mtandao ya kijamii kulisambaa taarifa iliyonesha moja ya mabasi ya abiria ya kampuni hiyo likitekea kwa moto katika maeneo ya Tanga mjini mkoani humo.

Akizungumza na www.eatv.tv kamanda Edward Bukombe amesema ni “ajali tu gari ilipata hitilafu gari likapata moto, mpaka dakika hii chanzo cha ajali kinaendelea kuchunguzwa, na ajali haikuwa na madhara kwa binadamu ila gari ndilo lilikuwa Linaelekea kubeba abiria".

Aidha kamanda huyo amekanusha taarifa ya kuwa gari hiyo ilikuwa imewaka moto eneo la kituo cha mafuta, na kusema kuwa gari lilikuwa likitoka kwenye eneo la kulaza magari kuelekea kituo cha mabasi yaendayo mikoani kwa ajili kuanza safari zake za kila siku.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad