China Kutengeneza Mwezi wao, Utakuwa na Uwezo wa Kutoa Mwanga Mara Nane ya Huu Uliyopo


Wanasayansi wa China wapo katika mipango ya kutengeneza Mwezi ambao utakuwa na uwezo wa kutoa mwanga mara nane ya huu uliyopo sasa huku ukitarajiwa kufungulia rasmi mwaka 2020. 

Utekelezaji wa mipango hiyo tayari imeshaanza kwakupitia ‘Chengdu Aerospace Science and Technology Microelectronics System Research Institute Corporation and the institute’ ambao tayari wamethibitisha kuwa wameshaanza kupiga hatua katika hilo. 

Kwa mujibu wa ‘mediaPeople’s Daily,’ mwezi huo feki utaangazia mitaa ya Chengdua na maeneo jirani ambayo yatakuwa na umbali kati ya kilomita 10 hadi 80 na utakuwa na uwezo wa kutoa mwanga wa kutosha utakaochukua nafasi hata wa ule mwanga uliyopo mitani. 

Wu Chunfeng, ambaye ni mwenyekiti wa Chengdu Aerospace Science and Technology Microelectronics System Research Institute Corporation, amesema kuwa Mwezi huo utaweza kutoa mwanga hata umbali umbali wa kilomita 50 kwenye maeneo ya Chengdu nyakati za usiku na kuweza kusaidia kuokoa dola za Kimarekani milioni 240 ambazo ni sawa na Yuan bilioni 1.2 ambayo inatokana na gharama ya umeme kila mwaka. 

Wanasayansi na wanamazingira wanahofia juu ya mipango hiyo, Mkurugenzi wa Sera ya Umma katika Chama cha Kimataifa kinachohusiana na anga giza, John Barentine ameiyambia Forbes kuwa licha ya mipango hiyo kutatua changamoto za Chengdu lakini itasababisha matatizo makubwa ya mazingira na kunauwezekano wa kuongezeka kwa uchafu wa mwanga.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad