Cristiano Ronaldo Amekana Madai kuwa Alibaka Mwanamke Mmoja Marekani Mwaka 2009



Ronaldo alijiunga na Juventus ya Italia kwa pauni milioni 99.2 akitokea Real Madrid mapema mwaka huu.

Cristiano Ronaldo ametupilia mbali madai ya mwanamke mmoja nchini Marekani ambaye anadai kuwa Ronald alimbaka mwaka 2009.

Kwenye video ya Instagram Ronaldo alisema: "Wanataka umaarufu kwa kutumia jina langu. Hiyo ni kawaida."

Mawakili wa Ronald wanasema wanalishtaki jarida la Ujerumani la Der Spiegel lililoripoti kwanza madai hayo.

Jarida hilo lilindika kuwa Kathryn Mayorga alikuwa amedai Ronaldo 33, alimbaka kwenye chumba kimoja cha hoteli huko Las Vegas.

Bi Mayorga, 34, anaripotiwa kuandika taarifa ya kubakwa kwa polisi wa Las Vegas muda mfupi 
Mwaka 2010 anaripotiwa kufikia makubaliano na Ronaldo ya malipo ya dola 375,000 ili asifichue madai hayo.

Mawakili wake sasa wanataka makubaliano y kutofichua madai hayo yatupiliwe mbali.

Ronaldo alijiunga na Juventus ya Italia kwa pauni milioni 99.2 akitokea Real Madrid mapema mwaka huu.

Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ureno anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi kipindi hiki duniani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad