Dar Yaongoza Matokeo Darasa la Saba

Dar Yaongoza Matokeo Darasa la Saba
Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Charles Msonde ametangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi huku kukiwa na ongezeko la ufaulu katika masomo ya Maarifa ya jamii, Sayansi, Hisabati na Kiingereza na ufaulu wa  somo la Kiswahili umeshuka ukilinganisha na wa mwaka jana.



Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwakufanya vizuri kati ya mikoa 10 bora kitaifa kiufaulu kwa kuwa na watahiniwa waliopata alama nyingi kwenye masomo matano. Ukifuatiwa na Geita, Arusha, Kilimanjaro, Kagera, Mwanza, Iringa, Mtwara, Katavi na Njombe.

Ambapo Baraza hilo pia limefuta matokeo yote ya wanafunzi 357 waliobanika kuhusika na udanganyifu na kuzuia kutoa matokea ya watahiniwa 120 ambao walikuwa wakiumwa na watafanya mtihani mwaka 2019.

Kwa mujibu wa NECTA, ufauli katika masomo ya English Language, Maarifa ya Jamii, Hisabati na sayansi umepanda kwa asilimia kati ya 4.03 na 11.92 ukilinganisha na mwaka jana, Huku ufaulu katika somo la Kiswahili ukishuka kwa asilimia 1.44.

Kwa mwaka huu, watahiniwa wavulana 27,559 ikiwa sawa na 6.17% wamefaulu kwa kupata daraja ‘A’ huku wasichana 19,781 ikiwa ni sawa na 3.98% Aidha waliopata daraja ‘B’ wavulani ni 145,075 sawa na 32.46% na wasichana wakiwa jumla yao 136,166 sawa na 27.47%.

Kuangalia matokeo ya darasa la saba mwaka 2018/19 bofya hapa

Baraza hilo pia limewatangaza walimu na maafisa waliohusika katika wizi wa mitihani ya darasa la saba pamoja na kufanya udanganyifu. NECTA imesema chimbuko la wizi lilipoanzia katika kituo teule cha kuhifadhia mitihani cha Nyanduga Rorya Mkoani Mara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad