Dreamliner Yashindwa Kuipeleka Taifa Stars Cape Verde.....Serikali Yakodi Ndege Nyingine

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku wa leo October 9 2018 itasafiri kuelekea Cape Verde kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2019 nchini Cameroon. Taifa Stars awali walikuwa wasafiri na ndege ya Air Tanzania Dreamliner lakini imeshindikana.

Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe amethibitisha kuwa  Dreamliner haiwezi kwenda na badala yake wamekodi ndege nyingine maalum kwa ajili ya safari hiyo.

Dreamliner imeshindwa kwenda kutokana na uwanja wa ndege waliopaswa kutua kuwa mdogo na hauwezi kupokea ndege kubwa kama Dreamliner.

“Tulimtuma Mgohi aweze kuangalia namna sehemu ilivyo tutakavyofikia, ametuambia kwamba uwanja ni mdogo kwahiyo tumeongea na wenzetu wa Airt Tanzania na tumeagiza ndege nyingine ambayo ina usajili wa Tanzania ambayo ina weza kushuka na kupaa kiurahisi,” alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad