Ebitoke aondoka Rasmi kwenye kundi lake

Ebitoke aondoka Rasmi kwenye kundi lake
Mchekeshaji ambaye amejizolea umaarufu mkubwa mtandaoni hivi karibuni, Ebitoke ameondoa kwenye kundi lake la Timamu.

Kwenye kundi hilo Ebitoke aliweza kushirikiana na wachekeshaji wengine kama Bwana Mjeshi Mr. Beneficial na Mamaa Ashura ambaye kitambo hajaonekana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ebitoke ameeleza kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia mkataba wake na Timamu TV kumalizika hivyo anaondoka na kuanza kufanya kazi sehemu nyingine.

"Napenda kuchukua nafasi hii na kuwatarifu Mashabiki na watu wote wanaonitazama na kusoma ujumbe huu, kuanzia sasa nitakua nikifanya kazi zangu nje ya Timamu TV, nikimaanisha mkataba wangu umeisha," ameeleza Ebitoke.

Pia utakumbuka ni mwaka huu ambao Ebitoke amecheza movie yake ya kwanza tangu kuanza kuigiza inayokwenda kwa jina la Sema ndani ya kundi hilo na uzinduzi wake wa awali ulifanyika Serena Hotel, Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad