Esha Buheti Afunguka na Kueleza Jinsi Mtoto Wake Alivyoiokoa Ndoa Yake

Esha Buheti Afunguka na Kueleza Jinsi Mtoto Wake Alivyoiokoa Ndoa Yake
Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Esha Buheti amefunguka na kuweka wazi jinsi mtoto wake wa mwisho aliyemzaa alivyoikoa ndoa yake.

Esha amedai mtoto wake aitwaye Claribel ameweza kwa asilimia kubwa kuiokoa ndoa yake ambayo alikuwa kabisa anaiona kama imeshavunjika na kukosa kabisa matumaini ya Kurudi tena.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Esha amesema kila akimuangalia mtoto wake huyo anakuwa na sababu nyingi za kumshukuru Mungu, kwa kuwa ndiye chachu ya kumfanya awepo kwenye ndoa yake mpaka leo.

Unajua kabla ya ujauzito wa mtoto wangu huyu ndoa yangu ilikuwa haina uhai kabisa yaani ilishikiliwa na uzi mdogo sana, lakini Mungu alipomleta mwanangu huyu na ndoa yangu ikarudi upya kabisa, nashukuru kwa hilo nina maelewano vizuri na mume wangu”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad