Fahamu Kwanini Instagram ilizimwa Kwa Muda Oct 03 2018


Baada ya mtandao wa Instagram kuzimwa, Jumatano ya Oktoba 3, kwa takribani saa moja na kulikopelekea mamilioni ya watumiaji wake kushindwa kutumia mtandao huo, hatimaye vyanzo mbalimbali vimetaja sababu zilizopelekea kuzimwa kwake.


Watumiaji mbalimbali walionekana kuchangia mada hiyo kwa kutumia msemo maarufu 'Hashtag' iliyokwenda kwa jina la '#INSTAGRAMDOWN' ambao wamesema mtandao huo ulizimwa kutokana na marekebisho mapya yaliyofanyika katika programu hiyo, mabadiliko ambayo yalionekana siku moja baada ya mtandao huo kurudi hewani.

Moja ya watu walioathirika ni pamoja na mdau mkubwa wa mitandao ya kijamii nchini, Dj Choka ambaye amesema,

_“binafsi natumia Instagram kufanya biashara na makampuni mbalimbali, lakini baada ya kustopishwa kwake imenifanya nimekosa kazi kama tano hivi za kampuni tofauti tofauti na natumaini wapo watu wengi waliopoteza hadi zaidi ya milioni 1 ndani ya muda huo”_.

Chanzo kingine ni kutoka kwa watumiaji wa mtandao wa Facebook ambao wamesema kuwa Instagram ilifungwa baada ya kutokuwa na maelewano mazuri ya kibiashara baina ya viongozi na wamiliki wa mtandao huo ambao kwa sasa mamejiuzulu nyadhifa zao.

Siku chache zilizopita kabla ya kutokea kwa tukio hilo, Facebook ilimtangaza kiongozi mpya wa mtandao huo, Bw. Adam Mosseri muda mchache baada ya waliokuwa waanzilishi na miongoni mwa wamiliki wa mtandao wa Instagram, Kevin Systrom na Mike Krieger kujitengua nyadhifa zao na kubaki kuwa watumiaji wa kawaida. Awali Bw. Mosseri alikuwa makamu wa rais wa uzalishaji wa Facebook.

Instagram ilinunuliwa na Facebook kwa dola bilioni 1 mwaka 2012, ambapo takwimu za sasa zinaonesha mtandao huo unatumiwa na watu zaidi ya bilioni moja kwa mwezi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad