Haji Manara ameelezea story yake ya kuwahi kunusurika kuzama katika kisiwa hicho za Mbudya enzi hizo bado mdogo na kusema kuwa alitoa shahada ya sala na ndipo alijikuta ufwekeni na tokea hapo maji anayoyafahamu ni ya kunywa na kuoga tu.
“Rafiki zangu wengi nishawahi kuwasimulia mkasa wangu na kisiwa cha Mbudya udogoni nikiwa na wazazi na ndugu zangu nilikaribia kuzama pale wakati nikiogelea nilifundishwa madrasa utotoni kabla ya kufa utoe Shahada Na nilishaisema kumaliza tu shahada ( لا إله الا ّالله Ù…Øمد رسول الله )”
“Nikajikuta maji yamenisukuma ufukweni toka siku hiyo maji nayajua ya kunywa na kuoga bafuni tu kuogelea mwisho maji ya UgokoYasemwa kifo cha kwenye maji na cha moto ni vifo vibaya zaidi na mwenzetu ametangulia mbele ya haki .Tumuombee Maghfira na cc Tujiombee Mwisho Mwema”