Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameamua kufunguka kuhusiana na namna kiungo wa Yanga, Ibrahim Ajib namna alivyoanzisha mpira kwa kuutoa nje.
Ajib alianzisha mpira huo kwa kuutoa nje baada ya Mwamuzi wa kati, Jonesi Rukiya kupuliza filimbi kuahsiria mwanzo wa dakika 45 za kwanza katika mechi dhidi ya watani zao wa jadi Simba.
Kitendo hicho kimemshangaza zaidi Manara akieleza kuwa hajawai kuona popote pale duniani katika mchezo wa soka kwa mchezaji kuanzisha mpira kwa kuutoa nje.
Manara ameeleza kuwa anajua ni vigezo na masharti ambayo alipewa mchezaji huyo jambo ambalo lilipelekea kuutoa mpira nje badala ya kumuanzishia mwenzake.
"Ibrahim Ajibu Migomba dunia inajua na wewe unajua namna nnavyoikubali miguu yako, na kwangu mim kando ya Kakolanya wewe ndiyo manusura yao leo, maana hapo si bahati mbaya, ni yale masharti na vigezo"
"Nimeangalia mechi za mpira na kwenye TV zaidi ya elfu kumi sijawahi ona hii ya leo, napingana hapa iwekwe kwenye Guinness World Records Book". aliandika.
ni kawaida yako kusema kuwa ni mara ya kwanaza kuona baadhi ya matukio huku ukijisahaulisha yaliyopita, kwa hiyo na refa alienda kwa mganga ili ampe mpira aanzishe ajibu? umri wako haufanani na unayofikiri ww mzungu.
ReplyDeleteAcheni kwenda na matokeo uwanjani itawagharimu sana