Halima Mdee Afunguka Chanzo cha Wabunge Kukimbilia CCM

Halima Mdee Afunguka Chanzo cha Wabunge Kukimbilia CCM
Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee amefunguka kuwa kinachopelekea wabunge wa chama chake kuhamia CCM ni tamaa zinazowaingia pindi wanapopewa dhamana na wananchi ya kuwatumikia na kudhani kwamba ubunge ni chanzo cha utajiri.


Akizungumza katika mahojiano maalum na www.eatv.tv Mdee amefunguka kuwa wabunge wote waliohama ni wale waliokimbilia kuchukua mikopo mikubwa bungeni na kupelekea kukatwa mishahara yote, kwahiyo kufanya vile ni kwaajili ya kunusuru hali zao kiuchumi.

"Kama wewe ni maskini kabla ya kuwa mbunge huwezi kuwa tajiri kwa miaka mitano", amesema Mdee.

Mdee ameongeza kuwa wabunge wamekuwa wakijiingiza kwenye biashara bila kuwa na ufahamu juu ya vitu husika wanavyokimbilia kufanya, hivyo wengine huishiwa pesa na kushindwa kuhudhuria vikao vya bunge jijini Dodoma.

"Wanakosa uelewa juu ya dhamana waliyopewa na wananchi, matokeo yake wanaishia kukopa mikopo mikubwa hadi wanakosa hela za nauli wengine, mfano Waitara na huyo Ryoba wamepiga watu vizinga hadi wameamua kufika bei, CCM sio wao ni ugumu wa maisha", amesema Mdee.

Usiku wa Septemba 27, aliyekuwa Mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Chacha alitangaza kujiuzulu uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini na kusema kuwa amechukua uamuzi huo kumuunga mkono mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Chacha Marwa Ryoba anakuwa Mbunge wa nne kutoka CHADEMA kuhama na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwa nia ya kuwaletea wananchi maendeleo akiungana na Mwita Waitara, Julius Kalanga, na Godwin Moleli.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wanagawana mbao Jahazi lishatota we endelea kusubiri uzame nalo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad